BALOZI wa Tanzania nchini Sweden, Mobhare Matinyi aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Biashara kati ya nchi za Nordic na Afrika, uliofanyika jijini Oslo, Norway.
Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Andreas Motzfeldt Kravik, alisisitiza umuhimu wa nchi za Nordic na Afrika kuwa na sera rafiki za biashara na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati. Aliongeza kuwa bara la Afrika linabeba mustakabali wa dunia.
Washiriki wa mkutano huo walitoka sekta binafsi, jumuiya za wafanyabiashara, viongozi wa serikali, wanadiplomasia na mashirika mbalimbali kutoka duniani, ikiwemo Marekani.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























