Magazeti leo Oktoba 14,2025

JESHI la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo Askari wa wa Jeshi la Polisi Omary Mnandi (30) ambapo walitenda tukio hilo usiku wa kuamkia Oktoba 12, 2025 baada ya askari huyo kukosea gari na kuingia kwenye gari lao akiwa amelewa.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha,SACP Justine Masejo ambayo imeeleza,watuhumiwa hao walitenda kosa hilo usiku wa Oktoba 11,2025.

Ni katika baa iitwayo Simaloi iliyopo maeneo ya Kaloleni ambapo walimjeruhi mtuhumiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea umauti wake wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya Omary Mnandi (marehemu) kutokana na unywaji wa pombe ambao ulipelekea kukosea uhakika wa gari lake namba T. 402 CNC na kuingia kwenye gari namba T. 734 AXR la mmoja wa watuhumiwa hao na ndipo walianza kumshambulia.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news