CHUO Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), kikiwa chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimepongeza juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu, kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation-HEET Project).
Katika taarifa iliyotolewa Rasi wa Chuo Kishiriki cha Mkwawa, Profesa Method Semiono ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukizi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amesema kuwa mradi huo ni matokeo ya dhamira ya Serikali ya kuendeleza elimu ya juu ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi nchini.
Alisema kuwa mradi wa wa HEET ambao serikali ya Rais Samia umekuwa na Uwekezaji wa Kimkakati katika elimu nchini ikiwa unatekelezwa kwa miaka mitano (2021/2022–2025/2026) unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unalenga kuboresha ubora wa elimu ya juu nchini.
Profesa Semioni alisema kuwa kupitia mradi huo MUCE imetengewa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 8 (sawa na Shilingi Bilioni 18.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















