Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wana jukumu la msingi la kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika maadili ikiwemo kuzingatia mila na desturi za kitanzania zinazofaa.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu alipotembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii-Ruaha tarehe 16 Oktoba, 2025 mkoani Iringa.Felister ameeleza kuwa nidhamu katika jamii haipo tena na wimbi la mmomonyoko wa maadili limekua kubwa kwani vijana hawana hofu ya kutumia lugha zisizofaa hadharani na kwenye mitandao ya kijamii hata kwa watu waliowazidi umri.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























