Magazeti leo Januari 18,2026

Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Marco Gaguti amefunga rasmi zoezi la Medani la EX- MALIZA lililofanywa na Kuruti wa Kundi la 44/25 katika eneo la Msata tarehe 16 Januari 2026.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Meja Jenerali Gaguti amewataka Kuruti hao wanaotarajia kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi hivi karibuni kuwa waadilifu, kujituma na kuwa watiifu kwa nchi yao.

Kuruti walioshiriki zoezi, wametakiwa kuzingatia mafunzo ya nadharia na vitendo kama shambulio la kunuia, shambulio la kushtukiza na somo la doria huku akionyesha wazi kuwa zoezi limefanikiwa.

Dhamira ya Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ni kuona kuruti wote wanahitimu na kwenda katika maeneo mbalimbali watakayopangiwa kushiriki kulilinda taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here