JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watuhumiwa wanne wakiwa na jumla ya vipande 23 vya meno ya tembo, katika operesheni iliyoshirikisha askari wa Wanyamapori iliyoyofanyika Wilaya ya Kilombero na Mvomero ikiwa ni mikakati ya jeshi hilo kuimarisha usalama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,SACP Alex Mkama ameeleza kuwa,tukio hilo lililotokea Oktoba 12, 2025 katika Kijiji cha Sagamaganga kata ya Signal Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro.
Amesema,wamekamatwa Ernest Edwini Makali (53) mkulima mkazi wa Mbingu na Loyce Mwaka Luvanda (58) mkulima mkazi wa mkoani Iringa wakiwa na vipande 20 vya meno ya Tembo.
Aidha,Oktoba 13, 2025 katika Kitongoji cha Kimbwala kilichopo Kijiji cha Kisaki Wilaya ya Morogoro alikamatwa, Mongota Lugwasha Jisabu (27) mkazi wa Kimbwala akiwa na vipande vitatu vya meno ya tembo huku Athumani Sadiki Mtai (32) mkulima mkazi wa Kiduwe na Ayoub Zakaria Kasian (18) wakitiwa nguvuni Oktoba 15, 2025 katika Kijiji cha Kidudwe kilichopo Kata ya Mtibwa Wilaya ya Mvomero wakiwa na kichwa kimoja cha Mnyama Swala.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























