Watoto tisa wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio kwenye kambi maalumu ya matibabu ya siku mbili iliyomalizika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Upasuaji huo umefanywa na wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) la nchini Israel.Akizungumza na waandishi wa habari Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto, Stella Mongela alisema upasuaji huo ulifanyika kwa njia ya tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambao ni maabara maalumu inayotumia mionzi kutambua na kutibu magonjwa ya moyo.





















Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo












