Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, ameendelea na kampeni zake za lala salama wilayani Masasi, katika viwanja vya Soko la Mkuti, Masasi Mjini.
Akiwahutubia mamia ya wakazi wa Masasi, Mhe. Doyo ameahidi kuwa serikali yake, endapo atapewa ridhaa na wananchi, itarejesha reli ya Masasi, Dar es Salaam, ambayo ilisitisha shughuli zake mwaka 1972.Amesema kuwa reli hiyo ilikuwa uti wa mgongo wa uchumi wa kusini, na kufufuliwa kwake kutachochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. “Kupitia reli hii, wakulima wa korosho, na mazao mengine ya biashara wataweza kusafirisha bidhaa zao kwa gharama nafuu hadi masoko makubwa ndani na nje ya nchi,” amesema Mhe. Doyo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

































