Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), limetangaza orodha ya Waamuzi na Maofisa walioteuliwa kwa ya ajili ya AFCON nchini Morocco.
Waamuzi na maofisa hao wanatakiwa kuripoti jijini Cairo yalipo Makao Makuu ya CAF kati ya Novemba 21 kwa ajili ya kambi ya maandalizi kabambe ambapo Mashindano yanaanza Desemba mwaka huu.
Katika orodha hiyo Mwamuzi mmoja pekee kutoka Burundi Pacifique Ndabihawenimana ndiye ambaye ameorodheshwa huku Tanzania ikiambulia patupu.Kwa upande wa Mrundi Pacifique Ndabihawenimana hiyo itakuwa ni AFCON yake ya nne baada ya kuwa Mwamuzi katika mashindano ya mwaka wa 2019,2021 na 2023.










Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













