WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa tuzo kwa wanafunzi ambao ni washindi wa uandishi wa insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 huku ikiwasisitiza kutumia uwezo wao binafsi katika kuandika insha badala ya kutegemea matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba.
Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hizo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Hussein Omar amesema kuwa uandishi wa insha ni sehemu ya mafunzo na inawajengea wigo mpana wa kujifunza masuala muhimu yanayohusu jumuiya hizo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






























