Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemfungia mchezaji wa Klabu ya Young Africans, Ibrahim Abdullah (Bacca) kutoshiriki mechi tano kutokana na kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Mbeya City, Ibrahim Ame, tukio lililofanyika katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Jumanne ya Septemba 30, 2025 na kumalizika kwa sare ya 0-0.
TPLB imeeleza kuwa, rafu hiyo ilikuwa ya hatari na ingeweza kuhatarisha usalama wa mchezaji huyo.
Sambamba na hilo, Mwamuzi wa mchezo huo, Omary Mdoe kutoka Tanga, naye amepewa adhabu ya kukaa nje kwa mizunguko mitano ya Ligi Kuu kwa kushindwa kutafsiri sheria ipasavyo katika mchezo huo, hali iliyochangia kutochukuliwa hatua stahiki dhidi ya tukio hilo uwanjani.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
























