Kikosi cha Nane cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TANBAT 08), kinacholinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kimetunukiwa Nishani za Ulinzi wa Amani na Umoja wa Mataifa (UN) kutokana na mchango wake mkubwa katika operesheni ya kulinda amani nchini humo chini ya mwavuli wa MINUSCA.
Katika sherehe ya gwaride la heshima iliyofanyika tarehe 06 Oktoba 2025 mjini Berberati, wanajeshi zaidi ya 500 wa TANBAT 08 wametunukiwa nishani hizo ikiwa ni ishara ya kutambua michango yao katika kuwalinda raia, kusaidia shughuli za kibinadamu, na kuimarisha utulivu katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro.
Uvishwaji wa nishani hizo uliongozwa na Naibu Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa nchini CAR, Meja Jenerali Maychel Asmi, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



























