TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesitisha Kampeni za Uchaguzi wa kiti Ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, baada ya kupokea taarifa za kuuawa kwa Mgombea Ubunge wa Chama Cha Wananchi (CUF), Daud Wilbrod Ntuyehabi.
Taarifa kwa umma ya kusitisha uchaguzi wa Ubunge, Jimbo hilo, iliyotolewa na kusainiwa Oktoba 8,2025 na Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Siha, Marco Masue, inaeleza kuwa kutokana na kutokea kwa tukio hilo, Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Siha, umesitishwa kuanzia Oktoba 8,2025.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



























