Waziri ajiuzulu kwa tuhuma za kughushi vyeti vya chuo

ABUJA-Serikali ya Nigeria imepata mshtuko wa kisiasa baada ya Waziri wa Ubunifu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Geoffrey Uche Nnaji kujiuzulu Oktoba 7,2025 akikabiliwa na madai ya udanganyifu wa vyeti.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Nigeria,Waziri Nnaji kupitia barua yake ya kujiuzulu aliyoituma kwa Rais Bola Ahmed Tinubu ameeleza kusikitishwa na kampeni za kuumiza dhidi ya jina lake.

Amesema, uamuzi huo si kukiri hatia, bali ni kuchagua kulinda heshima ya mchakato wa kisheria na kuzuia usumbufu kwa serikali ya Rais Tinubu.

Rais Tinubu kupitia msemaji wake,  Bayo Onanuga amekubali kujiuzulu kwa waziri huyo huku akimshukuru kwa huduma zake na akimtakia mafanikio katika majukumu yake yajayo.

Madai dhidi ya Nnaji yaliibuka baada kudaiwa kuwasilisha cheti cha digrii cha Chuo Kikuu cha Nigeria (UNN) pamoja na cheti cha National Youth Service Corps ambavyo ni vya kughushi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news