ZANZIBAR-Zimesalia siku tano ili kila mmoja wetu aliyetimiza na kukidhi vigezo vya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenda kutumia haki yake ya kupiga kura kwa amani na utulivu.

Tunakwenda kufanya hivi,tukitambua kuwa kura zetu kwa mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Hussein Ali Mwinyi ni chombo muhimu cha kuleta maendeleo endelevu kote Unguja na Pemba.
Hivyo, kura yako ni kwa amani na maendeleo endelevu Zanzibar, kwani amani ni nguzo ya uchumi, utalii na uwekezaji, hivyo kila Mzanzibari anapaswa kulinda umoja na mshikamano kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Tukumbuke kuwa, maendeleo endelevu yataendelea kupatikana Zanzibar kwa kumchagua kiongozi sahihi na mwenye maono makubwa kwa Zanzibar ambaye ni Dkt.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa kutiki zingatia kuweka alama ya tiki kwake kama anavyoelekeza kwenye hizi picha hapa chini;



.jpg)


