Rais Dkt.Mwinyi aahidi maendeleo zaidi Zanzibar

ZANZIBAR-Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa sasa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa,Serikali ijayo imepanga kuiletea Zanzibar maendeleo makubwa zaidi kwa kuweka vipaumbele katika sekta muhimu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Uwanja wa Michezo wa Bumbwini Kidimni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa msingi wa maendeleo ya taifa ni kudumisha amani, mshikamano na utulivu wa kitaifa.

Katika hotuba yake, Dkt.Mwinyi amebainisha maeneo kadhaa ambayo Serikali ijayo ya CCM itayapa kipaumbele ikiwa atachaguliwa tena.
Miongoni mwa maeneo hayo ni kuendelea kuboresha skuli za kisasa na kuongeza viwango vya ufaulu kwa wanafunzi katika ngazi zote Zanzibar.

Pia,kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wote wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na juimarisha huduma za afya kwa kuendeleza ujenzi wa hospitali za mikoa.

Vilevile, ameahidi kukamilisha ujenzi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani, ambayo inatarajiwa kufungua fursa nyingi za kiuchumi kwa wananchi.

Dkt.Mwinyi amesema,Serikali imetenga shilingi bilioni 11 kwa ajili ya kuwafidia wananchi waliopisha ujenzi wa mradi wa bandari.

Pia, amesema maghala ya chakula kwa lengo la kudhibiti bei na kuhakikisha uhakika wa chakula nchini yatajengwa.
Katika kuelezea msimamo wa Serikali kuhusu kura ya mapema, Dkt.Mwinyi amewataka wananchi kupuuza propaganda na upotoshaji unaoenezwa,akisisitiza kuwa ni haki ya kikatiba kwa vikosi vya ulinzi na usalama kupiga kura mapema.

Dkt.Mwinyi amwaomba wananchi kumpa ridhaa ya kuendelea kuongoza na kuwataka wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi ili kukipa ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi.
Wakati huo huo, baadhi ya wanachama kutoka vyama vya upinzani, hususan ACT Wazalendo, wamerejesha kadi zao na kujiunga na CCM, wakieleza kuwa "Zanzibar haina mbadala wa Dkt. Mwinyi" katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news