Rais Dkt.Mwinyi akutana na Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya AU

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mazungumzo na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AUEOM), ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Botswana, Mhe. Mokgweetsi Masisi Ikulu, Zanzibar akiongozana na ujumbe wa AUEOM.
Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amewakaribisha waangalizi hao na kuwahakikishia kuwa hali ya ulinzi na usalama kwa upande wa Zanzibar ni shwari na Zanzibar imejipanga na iko tayari kwa uchaguzi.
Nao ujumbe wa AUEOM umeeleza kufurahishwa na mjumuisho wa makundi maalum ya jamii katika shughuli za uchaguzi na ni matumaini yao kuwa, shughuli zote za uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar zitafanyika kwa kufuata sheria na taratibu zote, jambo litalorahisisha utekelezaji wa majukumu ya misheni hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news