ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SEOM) Ikulu, Zanzibar.

Ujumbe huo unaoongozwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Malawi, Mhe. Richard Msowoya ambapo amemweleza Mheshimiwa Rais Mwinyi kuwa SEOM imejipanga kupeleka wajumbe wake katika maeneo yote visiwani Zanzibar.










