ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) waliofika Ikulu Zanzibar leo Oktoba 20, 2025 kwa ajili ya mazungumzo naye.
Ujumbe huo umeongozwa na Naibu Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Dkt. Khamis Khalid Said, akiambatana na Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano na Habari, Bi. Christina Musarache.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamewasilisha kwa Rais Dkt. Mwinyi taarifa kuhusu shughuli za Tume ya Taifa ya UNESCO pamoja na maandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa UNESCO unaotarajiwa kufanyika nchini Uzbekistan kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 13,2025.






