ARUSHA-Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla mapema asubuhi ya leo Oktoba 29,2025 amewaongoza wananchi wa mkoa wake, kupiga kura kwa kutimiza wajibu wake na kutumia haki yake ya Kikatiba ya kuchagua viongozi.
CPA Makalla ameendelea kuwahakikishia wananchi wote hali ya usalama ya mkoa huo ni shwari na kuwataka wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kutimiza haki yako ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Aidha, CPA Makalla ametumia muda huo kuwahamasisha wanaArusha wenye sifa kujitokeza kupiga kura huku akiwathibitishia wananchi wote kuwa, wasimamizi wa uchaguzi wameweka utaratibu mzuri kwa kuwa na vituo na sehemu nyingi za kupigia kura, sehemu zinazomuwezesha mpiga kura kutotumia muda mrefu kusimama kituoni."Mimi mwenyewe nimeshatimiza wajibu wangu, vituo tayari viko wazi, kuanzia saa 01:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni, nimefurahi utaratibu ni mzuri hakuna foleni kubwa vituo ni vingi hivyo mtu akifika kituoni hatatumia muda mrefu, kila mtu atumie muda huo kwenda kwenye kituo alichojuandikisha,"amebainisha CPA Makalla.
