DAR-Nyota wa timu ya Taifa ya Taifa Stars na nahodha wa Klabu ya Simba SC, Shomari Kapombe ametajwa kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2025.
Ni katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kwa wachezaji wa ndani inayowaniwa pia na mshambuliaji wa Pyramids FC, Fiston Kalala Mayele.
Kapombe ndiye mchezaji pekee kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara kupenya kwenye 10 bora huku wachezaji wengine wote wakitokea Ligi za Morocco, Misri na Algeria.
Wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na mshambuliaji wa Al Ahli ya Libya, Ismail Belkacemi, beki wa Pyramids, Mohamed Chibi, mshambuliaji wa RS Berkane, Oussama Lamlioui,kiungo wa Pyramids, lbrahim Blati Touré.
Aliyekuwa beki wa RS Berkane, Issoufou Dayo ambaye ametimkia Umm Salal Sc ya Qatar na winga Emam Ashour wa Al Ahly.
Vilevile aliyekuwa winga wa Pyramids, Ibrahim Adel ambaye ametimkia Al Jazeera Fc ya Saudi Arabia na nahodha wa AS FAR Rabat,Mohamed Hrimat.
