Simba SC yaichapa Nsingizini Hotspurs mabao 3-0

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Simba SC ya Tanzania imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza umepigwa leo Oktoba 19,2025 kwenye Uwanja wa Somhlolo nchini Eswatini.

Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu huku Simba Sports Club chini ya Meneja wao na Kocha Mkuu Dimitar Pantev wakifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi.
Aidha,bao la kwanza katika mchezo huo lilipatikana dakika ya 45' kupitia kwa mlinzi Wilson Nangu baada ya kupiga shuti hatari lililomshinda kipa wa Hotspurs.

Kipindi cha pili kilishuhudia kasi ya Simba ikizidi kuongezeka ambapo Kibu Dennis Prosper alionyesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao mawili dakika ya 83 na 90, na kuhitimisha karamu ya mabao kwa Wekundu wa Msimbazi.
Kwa matokeo hayo, Simba SC sasa ina nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi, kwani itahitaji kulinda tu ushindi huo katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Oktoba 26, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo inahitaji sare yoyote au hata kupoteza kwa tofauti ya mabao mawili ili kufuzu rasmi hatua inayofuata ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Ushindi huu ni ishara ya maandalizi mazuri chini ya Meneja wao na Kocha Mkuu Dimitar Pantev na uimara wa kikosi cha Simba SC kinachoonekana kuwa na dhamira ya kurejea kwenye hatua ya juu ya soka la Afrika, ambapo wamewahi kufika nusu fainali na robo fainali katika misimu ya hivi karibuni.
Mchezo wa marudiano unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania, huku matarajio yakiwa ni kuona Simba SC ikiendeleza rekodi nzuri ya nyumbani na kuhitimisha kazi waliyoiweka ugenini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news