ANJOUAN-Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu amewahahakikishia wananchi wa Comoro kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana nao katika Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa wataalamu wake.
Balozi Yakubu ameyasema hayo wakati wa hafla ya kufunga Kambi Tiba iliyofanyika katika Hospitali ya Bambao ambapo ilielezwa kuwa, jumla ya wagonjwa 3,653 wamepatiwa huduma za matibabu na kati yao 20 walifanyiwa upasuaji muhimu kunusuru afya zao.
Gavana wa Kisiwa hicho,Dkt.Zaidou Youssouf akiambatana na Mshauri wa Rais wa Comoro (Siasa),Mheshimiwa Humed Msaidie aliahidi kutembelea Tanzania mwezi Januari,2026 ili kuweka sawa makubaliano ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na utaratibu bora wa kesi za rufaa kwa wananchi wa Anjouan.Kwa upande wake,mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Tanzania,Dkt.Asha Mahita alieleza kuwa, fursa za ushirikiano katika mafunzo na usambazaji wa dawa na vifaa tiba ni miongoni mwa vipaumbele vya kuzingatiwa kwa sasa.













