Tanzania yashiriki mjadala kuhusu matumizi ya Akili Unde (AI) katika kukuza usimamizi wa uchumi wa kikanda

NA CHEDAIWE MSUYA
WF Washington

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameshiriki katika Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), kilichojadili fursa na changamoto za matumizi ya Akili Unde (AI) katika usimamizi wa uchumi jumla kilichofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington DC, Marekani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting - CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

MEFMI ni taasisi ya kikanda inayolenga kujenga uwezo wa nchi wanachama katika usimamizi wa sera za uchumi jumla, masuala ya fedha, usimamizi wa madeni, pamoja na takwimu za kiuchumi.Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Dkt. Fred Msemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Kitaifa wa Tume hiyo, Bi. Angela Shayo, wakifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting - CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

Majadiliano ya kikao hicho yalijikita katika kuchunguza namna AI inaweza kuchangia katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, uchakataji wa taarifa kwa ajili ya maamuzi ya kisera na uwekezaji, upangaji na ugawaji wa rasilimali fedha, pamoja na utoaji wa huduma kwa umma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting - CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

Aidha, kikao hicho kilibainisha changamoto zinazokabili utekelezaji wa teknolojia ya AI katika nchi zinazoendelea, ikiwemo uhaba wa miundombinu thabiti, ukosefu wa takwimu sahihi, upungufu wa wataalam wenye umahiri wa kiteknolojia, na masuala yanayohusu usalama na usiri wa taarifa.

Kwa pamoja, nchi wanachama zilikumbushwa umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali, kujenga uwezo wa kitaasisi na kitaalam, pamoja na kuandaa sera na miongozo itakayohakikisha matumizi salama, yenye maadili na uendelevu wa teknolojia ya AI.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha wakifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting - CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Washington DC, Marekani).

Matumizi sahihi ya AI yana uwezo mkubwa wa kuimarisha usimamizi wa uchumi, kuongeza ufanisi wa taasisi, na kuiwezesha Afrika kusonga mbele katika kukuza uchumi shindani na jumuishi kwa manufaa ya wananchi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news