Upendo wa vijana kwa Dkt.Mwinyi kuelekea Uchaguzi Mkuu,wapo tayari kumpa kura za kutosha Zanzibar

ZANZIBAR-Kijana maarufu mtandaoni na Mpigaji Makachu Zanzibar, Aladini alikuwa haamini macho yake alipopata nafasi ya selfie na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi. 

Dkt.Mwinyi pia ni mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hii kwa Aladini ni kumbukumbu ya maisha yake, na kwa sababu ya upendo wake kwake akaamua achapishe picha hiyo kwenye tisheti yake.
Kijana Maarufu mtandaoni na Mpigaji Makachu Zanzibar, Aladini akiwa amevalia tisheti yenye Selfie ya Rais Dkt.Mwinyi ambayo aliichapisha baada ya kuipiga hivi karibuni akiwa pamoja na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Tukio hili, linatufundisha mambo mengi kutoka kwa Rais Dkt.Mwinyi, mosi ni aina ya uongozi wake wa kuwa karibu na wananchi.

Ikumbukwe kuwa, Rais anapoamua kupiga selfie na mwananchi wa kawaida, anaonesha kuwa anajiona sehemu ya watu, siyo mtu wa kutengwa na ulinzi au mamlaka.

Hii hujenga imani na ukaribu, na watu huhisi wako karibu na Serikali yao, na ndivyo ilivyo kwa Serikali ya Awamu ya Nane tangu iingie madarakani mwaka 2020.

Rejea, Rais Dkt.Mwinyi alianzisha mfumo wa mawasiliano wa kuwezesha wananchi kuwasilisha hoja, kero na pongezi moja kwa moja kwake.

Mfumo huo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR) unawezesha wananchi kupiga simu au kutuma ujumbe kwa njia ya tovuti.

SNR limekuwa jukwaa muhimu kwa wananchi kuwasilisha kero zao na kupatiwa ufumbuzi wa haraka, ambapo Dkt.Mwinyi ni kiongozi wa kwanza nchini kuanzisha utaratibu huu unaowaleta wananchi karibu.

Pili,katika jamii nyingi, viongozi huonekana kuwa mbali au wa heshima ya hali ya juu kiasi kwamba ni vigumu kuwasogelea, lakini kwa Rais Dkt.Mwinyi ni tofauti kabisa, kwani licha ya kuwapa nafasi wananchi kupiga picha za namna hii amekuwa akijumuika nao moja kwa moja katika shughuli za kijamii, kuwatembelea katika makazi, biashara zao na hata kwenye ibada amekuwa akijumuika nao mara zote.

Ukaribu huo umewezesha Serikali kuzipatia ufumbuzi wa haraka changamoto zinazowakabili wananchi huku ikitekeleza miradi mingi inayogusa maisha ya wananchi wote, tembea kote Unguja na Pemba utabaini kuwa, maendeleo yaliyopatikana ndani ya miaka mitano chini ya Rais Dkt.Mwinyi yanafurahisha.

Kwa hiyo,Selfie kama hii huonyesha kuwa heshima si lazima iwe kwa misingi ya hofu, bali kujenga urafiki, mawasiliano ya moja kwa moja na unyenyekevu.

Tatu, kitendo cha Rais kupiga picha na wananchi wa kawaida huonesha kuwa kiongozi hana kiburi, anathamini kila mtu, na yuko tayari kutumia muda wake na wananchi bila kujiona yupo juu kuliko wengine.

Pia,katika enzi hizi za kidigitali, picha ya pamoja hasa selfie ni njia bora ya mawasiliano na vijana.

Inafundisha kuwa viongozi wanapaswa kwenda waliko watu hasa mitandaoni, ambako ndiko sauti za wengi zinasikika leo.

Kwa ujumla, selfie hii na Rais Dkt.Mwinyi haikuwa tu picha bali ulikuwa ni ujumbe wa uongozi bora, wenye kujali utu,wa kisasa,wa kibinadamu na unaogusa maisha ya watu moja kwa moja bila kujali nafasi zao katika jamii. 

Ndiyo maana kura yangu mimi na wewe Oktoba hii, itampa ushindi wa kutosha Dkt.Hussein Ali Mwinyi aendelee kuleta maendeleo zaidi Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news