Uwanja wa Uhuru wafikia asilimia 90 ya marekebisho

DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amefanya ziara ya kukagua Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambao umefikia asilimia 90 ya ukarabati.
Amefanya ziara hiyo Oktoba 13, 2025 akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Methusela Ntonda ambapo ukamilishaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuboresha miundombinu ya michezo nchini.
"Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu ukarabati huo ili kuhakikisha viwango vya kimataifa vinazingatiwa na lengo ni kuona uwanja huu unarejea katika hadhi yake" alisema Msigwa.

Kati ya maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni pamoja na ufungaji wa taa mpya za kisasa, uwekaji wa nyasi bora za bandia (Pitch), marekebisho ya njia za kukimbilia (Running Track), ufungaji wa viti vipya, ukarabati wa vyoo, ufungaji wa milango mipya na uwekaji wa vigae vipya pembezoni mwa uwanja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news