DEREK Kaitira Murusuri ni mwandishi, mwanahabari, na mshauri wa maendeleo nchini Tanzania, anayeheshimika kwa maandiko na uchambuzi wake kuhusu ukombozi wa kiuchumi na uongozi barani Afrika.
Akiwa na uzoefu mkubwa katika masuala ya kisiasa, Derek Murusuri pia amejikita katika kazi za ushauri, utafiti na mafunzo katika nyanja mbalimbali za maendeleo na siasa ndani na nje ya Tanzania.
Mwaka huu alizindua kitabu kipya kinachochambua kwa kina falsafa ya uongozi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Kitabu chake kilichopewa jina la Samia na Falsafa ya Samiaolojia", kinachambua falsafa ya "4Rs" ya Rais Samia yaani Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi Upya kama nguzo kuu za uongozi wake.
Murusuri ameendelea kushiriki kikamilifu kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa, hususan katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania.