VIDEO:Namna ya Kutiki kwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi,kiongozi wa kazi,maendeleo na kiunganishi Zanzibar

NA DIRAMAKINI 

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kuimarisha taswira ya uongozi wa kisasa unaojikita katika kazi, maendeleo na mshikamano wa kitaifa, hatua inayowafanya wananchi wengi kumwelezea kama kiongozi wa kazi, maendeleo na kiunganishi Zanzibar.
Tangu achaguliwe kuongoza Zanzibar mwaka 2020, Dkt.Mwinyi ameweka msisitizo mkubwa katika kusimamia utendaji wa serikali kwa uadilifu, kuwajibisha watendaji wazembe na kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa manufaa ya wananchi.

Katika kipindi chake cha uongozi kupitia Serikali ya Awamu ya Nane, Zanzibar imepiga hatua kubwa katika sekta ya miundombinu, afya,elimu na uwekezaji.

Pia,Serikali yake imetekeleza miradi mikubwa ya barabara, uboreshaji wa huduma za maji safi na salama, pamoja na ujenzi wa vituo vya afya na hospitali za kisasa.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesifiwa kwa juhudi zake za kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kupitia maboresho ya mazingira ya biashara na uwekezaji visiwani humo.

Kupitia dira ya Zanzibar ya Viwanda,Serikali imeweza kuanzisha maeneo maalum ya kiuchumi (SEZs) yanayochochea ajira na uchumi wa visiwa hivyo.

Lakini si kazi tu na maendeleo yanayomtambulisha Dkt.Mwinyi, bali uwezo wake wa kuwaunganisha Wazanzibari wa itikadi tofauti ambao umemfanya kupewa sifa kama kiunganishi wa kweli wa jamii.

Kupitia uongozi wake, Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) imeimarika zaidi kwa ushirikiano wa vyama mbalimbali, hali iliyopunguza migawanyiko ya kisiasa na kuimarisha amani ya kudumu visiwani humo.

Rais Dkt.Mwinyi mara kadhaa amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa kitaifa, uwajibikaji na kupiga vita vitendo vya rushwa na ubadhirifu.

Anasisitiza kuwa,Zanzibar mpya ni ya wote. Hataki ubaguzi wala urasimu, anataka maendeleo yanayomgusa kila mwananchi bila kujali anatoka wapi kote Unguja na Pemba.

Kwa mafanikio haya, Dkt.Hussein Ali Mwinyi anaendelea kujenga historia ya kipekee kama mmoja wa viongozi walioliletea taifa mabadiliko chanya kupitia uongozi uliojengeka katika maono mapana, kazi thabiti na mshikamano wa kweli, hivyo Oktoba hii, tunapaswa kumpa kura za kutosha ili aendeleze alipoishia kwa ustawi bora wa jamii Zanzibar na nchi kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news