DAR-Wadau wa teknolojia jijini Dar es Salaam wamepata nafasi ya kutambulishwa kwa simu mpya ya Redmi 15C kutoka kampuni ya Xiaomi, katika kikao kilicholenga kuonesha uwezo na mwelekeo wa kifaa hicho sokoni.

Katika tukio hilo lilofanyika Dar es Salaam juzi, washiriki walipata nafasi ya kushuhudia kwa karibu vipengele vipya vya Redmi 15C pamoja na bidhaa nyingine ikiwemo Redmi Pad, sambamba na majadiliano kuhusu mustakabali wa matumizi ya teknolojia janjanja nchini.
Baadhi ya washiriki walijipatia zawadi mbalimbali kama ishara ya shukrani kwa kushiriki katika utambulisho huo, huku kampuni ikisisitiza dhamira yake ya kuendeleza uwepo wake na ushirikiano na watumiaji wa Tanzania.
Kwa mujibu wa waandaaji, tukio hilo liliandaliwa mahsusi kwa wadau ili kuonesha namna teknolojia mpya ya Redmi 15C inavyoweza kuendana na mahitaji ya jamii ya sasa yenye kutegemea zaidi mawasiliano na matumizi ya kidijitali.


