Yanga SC yavunja mkataba wa Kocha Romain Folz

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Young Africans Sc imetangaza kuvunja mkataba wa Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz ikiwa saa kadhaa baada ya klabu hiyo kupokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Silver Striker Fc ya Malawi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)
Taarifa ya leo Oktoba 18, 2025 iliyotolewa na Uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa, katika kipindi hiki kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Msaidizi Patrick Mabedi huku mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu ukiendelea.

“Uongozi wa Young Africans SC unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya Klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news