ZANZIBAR-Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limewatangazia wateja wake kuhusu kuendelea kwa kazi ya ujenzi wa njia mpya ya umeme, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu na kuongeza ubora wa huduma ya umeme visiwani.
Kutokana na kazi hiyo, ZECO litalazimika kuzima umeme kwenye baadhi ya maeneo ili kuruhusu utekelezaji salama wa shughuli hiyo. Umeme utazimwa kwa njia za msongo wa kilovolti 33 na 11, hasa kwa kuwa njia mpya inapita karibu na ile ya zamani inayosambaza umeme katika ukanda wa Kaskazini Unguja.
Taarifa ya ZECO imeeleza kuwa umeme utakatwa kesho Jumapili, tarehe 5 Oktoba 2025 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.
Maeneo yatakayoathirika ni: Mwanyanya, Bububu, Kwa Nyanya, Chuini, Mfenesini, Kitope, Mahonda, Donge, Mkokotoni, Tumbatu, Shangani Shamba, Kivunge, Fukuchani, Kidoti, Tazari, Kigunda, Mwambale, Kendwa, Nungwi, Kizimbani, Dole, Kianga, Masingini, Mtofaani, Hawai na Kinuni.
ZECO inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza na inawaomba wateja kuwa wavumilivu wakati zoezi hilo likiendelea kwa ajili ya huduma bora zaidi.
