Ajali ya basi yaua watano Monduli

ARUSHA-Watu watano wamefariki dunia huku mmoja akijeruhiwa baada ya magari mawili kugongana huko katika maeneo ya Mbuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 23, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP Justine Masejo.

Amesema, ajali hiyo imetokea majira saa saba mchana katika eneo hilo.

SACP Masejo amebainisha kuwa, ajali hiyo imehusisha basi la abiria la Kampuni ya Ngasere lenye namba za usajili T. 922 DZQ aina ya Yutong likitokea Dodoma kwenda Arusha na kugongana na gari ndogo lenye namba za usajili T. 705 DFP aina ya Mark X likitokea Arusha.

Waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume watatu na wanawake wawili, huku majeruhi akiwa ni mwanamke,ambao wote walikuwa ni abiria katika gari ndogo.

Pia, jeshi hilo limesema linaendelea kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo, ambapo majeruhi amelazwa katika Hospitali ya Jeshi Monduli kwa ajili ya matibabu, na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Makuyuni.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari na kufuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani wakati wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news