Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia masuala ya afya, Dkt. Jafari Rajabu Seif, amewataka watumishi wa afya nchini kuhakikisha wanatumia lugha ya upole na staha wanapowahudumia wagonjwa katika vituo vya afya na zahanati za Serikali.
Dkt. Seif ametoa wito huo wakati wa ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Afya cha Nyarugusu, kilichopo Kata ya Nyarugusu, Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
“Serikali ya Dkt. Samia itaendelea kuboresha huduma za afya, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya afya na zahanati. Hata hivyo, pamoja na maboresho hayo, nyinyi watoa huduma mna wajibu wa kumpokea mgonjwa kwa tabasamu na kutumia lugha safi, si lugha chafu,” amesema Dkt. Jafari.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

































