Bajeti ya Simba SC mwaka 2025/2026 ni shilingi bilioni 29

NA DIRAMAKINI

SIMBA Sports Club ya jijini Dar es Salaam imepanga kukusanya shilingi 29, 555,207,704 na matumizi shilingi bilioni 27,161,824,254 Kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kuijenga klabu hiyo ndani na nje ya uwanja.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha Simba Sports Club,Suleiman Kahumbu wakati akisoma ripoti ya mapato ya msimu uliopita kwenye Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika mapema leo Novemba 30, 2025 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Bajeti ya klabu hiyo kwa mwaka huo, ni ongezeko la asilimia 13.5 kutoka bajeti ya mwaka uliopita ambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 26.
Kahumbu amesema, Rais wa Heshima wa klabu hiyo na mwekezaji,Mohamed Dewji (Mo Dewji) alichangia kiasi cha shilingi bilioni 4 kwenye bajeti yao ya msimu uliopita.

Pia,amebainisha kuwa,katika bajeti ya msimu huu 2025-26, Mo Dewji amechangia shilingi bilioni 6 kwenye bajeti yao ya mwaka ujao wa fedha.
Katika hatua nyingine,Serikali imesisitiza kuwa haitalazimisha Klabu yoyote nchini kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji bila uamuzi wa wanachama wake, na kwamba jukumu lake kuu ni kuhakikisha mchakato wowote unaotekelezwa unaendana na Sheria za nchi pamoja na kanuni zinazoongoza mchezo wa mpira wa miguu.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ameyasema hayo wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa mwaka wa Klabu ya Simba uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mwinjuma amesema kuwa, hatima ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo iko mikononi mwa wanachama, na Serikali haina dhamira ya kuingilia maamuzi yao.
"Mchakato huu ni wenu; ni uamuzi wa wanachama. Kama mtakubaliana kuendelea, kutathmini upya au kubadili mwelekeo, basi uamuzi huo utaheshimiwa,” amesema Mhe. Mwinjuma.

Ameongeza kuwa, Serikali inatamani kuona mijadala na maamuzi kuhusu mustakabali wa klabu hiyo haitawaliwi na hisia bali busara, kuzingatia sheria, maslahi mapana ya klabu na mustakabali wa michezo nchini.
“Lengo letu ni kuhakikisha mjadala na maamuzi ya leo hayapotezi mwelekeo kutokana na hisia, bali yanaongozwa na busara, sheria, maslahi ya klabu na maendeleo ya michezo nchini,” amesisitiza Mhe. Mwinjuma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news