TANGA-Wananchi wa Mkoa wa Tanga wameendelea kuhamasishwa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kipindi cha maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Elimu hiyo imetolewa Novemba 29,2025 kupitia Korogwe FM katika Wilaya ya Korogwe na Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto, Inspekta Mahundi, ambaye aliambatana na Konstebo Rehema.
Inspekta Mahundi amefafanua maana ya maadhimisho ya siku 16, sababu za kuanzishwa kwake, aina za ukatili wa kijinsia, athari zake na hatua zinazopaswa kuchukuliwa na jamii ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Kwa upande wake, Konstebo Rehema amehimiza wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini viashiria vya ukatili, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya jamii na Dawati la Jinsia ni nguzo muhimu katika kuzuia madhara yanayoweza kuwapata wahanga.
