NA DIRAMAKINI
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeshiriki katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni (IFEM) kwa mujibu wa Sera ya Ushiriki katika Soko la Fedha za Kigeni ya mwaka 2023, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuimarisha utulivu wa masoko ya fedha.
Kupitia ushiriki huo,Benki Kuu imeuza Dola za Marekani milioni 25.00 kupitia mnada wa ushindani kwa kiwango cha wastani cha kubadilisha fedha za kigeni cha Shillingi 2,443.82 kwa Dola moja ya Marekani.
"Lengo la mnada huu lilikuwa ni kuongeza ukwasi katika soko la fedha za kigeni."

