Watoto sita miongoni mwa 10 duniani kote hawajui kusoma sentensi rahisi wala kusuluhisha maswali ya kimsingi ya hesabu licha ya theluthi yao kuwa shuleni kwa sasa.
Haya ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika linalofahamika kama People’s Action for Learning (PAL) Network iliyotathmini matokeo ya masomo miongoni mwa watoto 89,870 wenye umri wa miaka mitano hadi 16 katika mataifa 12.
Matokeo hayo yamezua wasiwasi mkubwa kuhusu ubora wa elimu katika mataifa mengi maskini kwa kufichua kwamba kuhudhuria shule pekee sio hakikisho la masomo halisi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






























