DIRAMAKINI yampongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa ushindi mkubwa Zanzibar

DAR-Leo Novemba 3,2025 3,2025 DIRAMAKINI imetoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa ushindi wake mkubwa katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29,2025 na kwa kuapishwa rasmi hivi karibuni.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Godfrey Ismaely Nnko,Mtendaji Mkuu na Mhariri wa Diramakini Business Limited (DIRAMAKINI), ameeleza kuwa, ushindi huo wa kishindo kwa Dkt.Mwinyi ni kielelezo cha imani kubwa ambayo wananchi wamempa kutokana na uongozi wake wa hekima, uzalendo, na dhamira thabiti ya kuwaletea maendeleo.

"Tuna imani kuwa chini ya uongozi wako,Zanzibar itaendelea kudumisha amani, umoja na ustawi wa kijamii na kiuchumi.

"Tunakuombea afya njema, hekima, na ujasiri katika kutekeleza majukumu yako makubwa ya kulitumikia taifa. Mungu aendelee kukupa nuru na nguvu katika safari hii ya kuiongoza Zanzibar.Hongera sana Mheshimiwa Rais."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news