Tazama Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alivyoapishwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima la uapisho mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa kwenye sherehe za uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Matukio mbalimbali katika sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Masaju akimuapisha Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 03 Novemba 2025.
Matukio mbalimbali katika sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Msumbiji Daniel Chapo pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025. Marais hao pamoja na viongozi kutoka nchi mbalimbali walihudhuria sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa kwenye sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa silaha za jadi Mkuki kutoka kwa Mzee Ndijina Ndilanza Ndilito, mwakilishi wa wazee wa Tanzania Bara pamoja na ngao kutoka kwa Bi. Ubwa Hamis Ally mwakilishi wa Wazee wa Zanzibar kama ishara ya kulinda na kuitetea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news