DODOMA-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM Taifa kilichofanyika jijini Dodoma leo Novemba 5, 2025.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.



