Je! Wajua kuwa pigo au kofi moja la Simba wakati wa kumdhibiti mnyama amuwindaye lina nguvu ya takribani kilogramu 181?

NA JACOB KASIRI

SIMBA ni mmoja wa wanyamapori wanaopendwa na kuheshimika zaidi duniani akijizolea umaarufu mkubwa kutokana na ujasiri na nguvu wakati wa kusaka mawindo yake, nguvu na ujasiri wake wa kuwinda wanyama wakubwa na wakali zaidi yake ndio uliopelekea kuitwa “Mfalme wa nyika.”
Nguvu hizo za kuwadondosha, kuwararua na kuwafanya vitoweo vya siku wanyama wakubwa zaidi yake ndio uliwahamasisha watafiti kupima uwezo wa nguvu za pigo au kofi lake wakati wa kumdhibiti mnyama aliyemnuia kumla. Hivyo pigo au kofi hilo moja lilitathimiwa na kuwa ni pauni 400 ambazo ni sawa na kilo 181.

Nguvu hizo ni sawa na mnyama kudondoshewa ghafla mafurushi zaidi 3 ya mchanga yaliyoviringishwa pamoja yenye uzito wa kilo 50 kila mmoja, ambapo madhara yake ni pamoja na mshituko wa ghafla kwenye mfumo wa fahamu wa mnyamapori anayewindwa na kupelekea kupoteza uwezo wa kujihami, mwelekeo na wakati mwingine kuzilahi.

Aidha, mchanganyiko wa kucha zake ndefu zenye zaidi ya sentimita 3, nguvu na uwezo wa kumuadaa adui wakati wa mawindo yake yameendelea kumfanya simba awe ni mnyamapori anayeogofya si kwa binadamu tu bali hata wanyamapori wenzie.

Kwa tathimini na uzoefu wa waongoza watalii (tour guides) kadhaa niliofanyanao mahojiano, walisema wageni hufurahishwa sana na kuridhika wanapowaona simba wakiwa katika mawindo yao au katika harakati zao za maisha tofauti na kutowaona kabisa.

Ni mkono upi kati ya wa kulia au wa kushoto una nguvu zaidi kwa simba?

Kwa simba dume ambao mara nyingi huwinda peke yao, mkono wa kushoto ndio hutumika zaidi wakati wa mawindo yake.

Lakini kwa simba jike hutumia mikono yote miwili kutokana na asili yao ya kuwinda kwa ushirikiano, na kitoweo kinapopatikana hula kwa pamoja.

Kwa habari kemkem za simba, idadi yao na kwanini simba jike wakiwinda na kuua, kama kuna dume pembeni ndilo huanza kula? Kwa hayo na mengine mengi kumuhusu simba tukutane - Hifadhi ya Taifa Ruaha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news