KILIMANJARO-Mabaki ya mwili wa Kijana Joshua Loitu Mollel aliyeuwawa nchini Israel na wapiganaji wa Hamas Oktoba 07, 2023 yamewasili leo Novemba 19, 2025 katika kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).
Mabaki ya mwili huo yamepokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiongozwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa na Balozi Silima Haji Kombo.


















