DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Novemba 19,2025 ameteua Bakari Machumu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Rais Ikulu
Pia, amemteua Bw.Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Masuala ya Habari na Mawasiliano na Bw. Lazaro Samuel Nyalandu ameteuliwa kuwa Balozi.

