SERIKALI ya Tanzania imewataka wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi nchini wawe tayari kurejea nchini mwao ambako imewahakikishia kurejea kwa hali ya amani na utulivu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alitoa msimamo huo wakati wa Mkutano wa 26 wa Pande Tatu baina ya Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) uliohusu urejeshaji wakimbizi katika nchi yao ya Burundi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
































