Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Tadesa Limoli (32) raia wa nchini Ethiopia na wenzake 37 wote wanaume kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo Novemba 11, 2025 huko katika Pori la ranchi ya Matebete lililopo katika Kijiji cha Igumbilo Shamba, Kata ya Chimala, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya wakisafiri kwa kutumia Gari yenye namba za usajili T.953 DJF aina ya Toyota Noah mali ya Stanslaus Mazengo [51] Mkazi wa Isitu ambaye ndiye alikuwa akiendesha Gari hiyo.
Mtuhumiwa Stanslaus Mazengo ameeleza kuwa alikuwa akiwapeleka kuwahifadhi Wahamiaji hao kwenye nyumba ya Jackline Malya [26] Mkazi wa Chimala. Watuhumiwa walikuwa wakiwasafirisha Wahamiaji hao kwa njia ya kificho kwa lengo la kuwapeleka nchini Afrika ya Kusini.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
















