MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,amewatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Mtera Dam katika Wilaya ya Mpwapwa na kuwapa pole kufuatia madhila ya kuunguliwa na Bweni hapo Novemba 12, 2025 na kupoteza kila kitu hali iliyoulazimu uongozi wa Wilaya hiyo kufanya utaratibu wa kuwahamishia kwenye shule mbili za Mazae na Kimaghai ili waweze kuendelea na masomo.

Mhe. Senyamule alifika shule moja wapo ya Mazae Novemba 13, 2025 akiwa ameambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu, Kamati ya Usalama Mkoa na Afisa Elimu Mkoa ambapo wametoa baadhi ya mahitaji muhimu yatakayowawezesha wanafunzi hao wa kike kuweza kuendelea na masomo yao pasi na changamoto yeyote.
Akizungumza na wanafunzi hao, Mhe. Senyamule amesema jambo jema la kumshukuru Mungu ni kwamba hakuna maisha ya mwanafunzi yeyote yaliyopotea zaidi ya vitu tu ambavyo vinaweza kutafuta ila uhai wa mtu hauwezi kutafutwa.












Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo










