Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema viongozi bora ni chachu ya utekelezaji wa mageuzi ya elimu nchini ambayo yatasaidia kupata wahitimu mahiri wenye uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya taifa.


Akizungumza Novemba 18, 2025 jijini Dodoma, Prof. Nombo amewapongeza viongozi wapya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Wanu Hafidh Ameir, akisema kuwa uteuzi wao na kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni ishara ya kuaminiwa kwa uongozi wao mahiri.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























