SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeufungia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mchezo huo.
Taarifa iliyotolewa Novemba 26, 2025 na shirikisho hilo, imesema miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu.“Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF. TFF inazikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja,” imeeleza taarifa hiyo.


.jpeg)

%20(1).jpeg)

.jpeg)
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













