Baada ya kuapishwa, Dkt. Nchemba ameahidi kuendeleza juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu, akisisitiza dhamira yake ya kuimarisha miradi ya kijamii na kiuchumi inayolenga kuinua ustawi wa wananchi wa Iramba Magharibi.
Wananchi wa Iramba Magharibi pamoja na Watanzania kutoka maeneo mbalimbali wameendelea kumpongeza kupitia mitandao ya kijamii, wakieleza imani yao kuwa ataendeleza uongozi wenye tija, uwajibikaji na matokeo chanya kwa Taifa.