Miradi ikamilike kwa manufaa ya wananchi-Profesa Shemdoe

NA JAMES MWANAMYOTO
OWM TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka watendaji walio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI na taasisi zake, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukamilishaji wa miradi ya maendeleo iliyopo katika hatua ya utekelezaji ili ikamilike kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akikisitiza jambo kwa Katibu Mkuu OWM - TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru , wakati kikao kazi maalum na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa ofisi hiyo.

Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo leo, wakati wa kikao kazi chake maalum na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara na Vitendo vya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI pamoja na Taasisi zote zilizopo chini ya ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akiongoza kikao kazi maalum na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa ofisi hiyo.

“Ni vema mkaona namna bora ya kukamilisha miradi inayotekelezwa ili iwanufaishe wananchi, hivyo hakikisheni miradi yote iliyoanzishwa inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi,” Prof. Shemdoe amesisitiza.

Aidha, Prof. Shemdoe ameelekeza kuangaliwa upya suala la ujenzi wa masoko ya ghorofa kwenye Halmashauri kama yanakidhi uhitaji, kwani uzoefu unaonesha kuwa wananchi hususani wajasiriamali hawapendi kufanya shughuli zao ghorofani.
Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Bw. John Cheyo, akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, wakati wa kikao kazi maalum cha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa ofisi hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Bw. Adolf Ndunguru akitoa neno la utangulizi wakati wa kikao kazi maalum cha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa ofisi hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) anayeshugulikia Elimu Mhe. Reuben Kwagilwa akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi maalum na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa ofisi hiyo.

“Mfano mzuri ni soko la Machinga Complex Dar es Salaam, ambapo wananchi wengi wanapanga bidhaa zao barabarani badala ya kutumia vizimba vilivyo ghorofani, hivyo tutathmini kama kuna haja ya kujenga masoko ya ghorofa?” ametoa angalizo Prof. Shemdoe.

Prof. Shemdoe ameshauri kuwa, iwapo itaafaa yajengwe masoko kama lililivyo la Machanga Complex Dodoma ambalo linawawezesha wafanyabiasha na wajasiriamali kujipatia kipato kwa kupanga bidhaa zao kwenye meza au vizimba walivyoandaliwa sokoni, na kuongeza kuwa hata gharama ya ujenzi wake ni ndogo ukilinganisha na ujenzi wa masoko la ghorofa.
Naibu Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Bw. Atupele Mwambene (wa kwanza kulia), Prof. Tumaini Nagu (katikati) na Mhandisi Rogatius Mativila (wa kwanza kushoto) wakiwa katika kikao kazi maalum cha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akiwa katika kikao kazi maalum na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa ofisi hiyo.

Prof. Shemdoe amefanya kikao kazi hicho maalum na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, ambapo ametumia kikao kazi hicho kuhimiza uwajibikaji utakaoiwezesha ofisi anayoisimamia kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora zitakazopelekea wananchi hususani wa kipato cha chini kupata tabasamu ndani ya nchi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news